ANZA

FANYA JARIBIO LA KUHUSU UNYWAJI SASA

ANZA

Unauelewa kiasi gani kuhusu pombe au vileo?

Ni kipi kati ya hivi kina kilevi zaidi?

Vyote viko sawa

Kipimo cha kawaida cha pombe kali, bia au wine (mvinyo), vyote vina kiwango sawa cha kilevi. Madhara kwenye mwili wako huchangiwa na kiasi unachokunywa na sio unachokunywa.

SWALI LINGINE

Ni madhara gani yanahusishwa na utumiaji wa pombe haramu?

Vyote viko sawa

Ununuzi wa pombe haramu unaweza kuhatarisha afya yako. Pombe haramu zinaubora hafifu na huzalishwa katika mazingira yasiyo safi. Zipo nje ya utaratibu wa udhibiti wa serikali, hazilipi kodi na mara nyingi huhusishwa na matukio ya kihalifu ambayo huathiri biashara halali.

SWALI LINGINE

Wanaume na wanawake wanaokunywa kiasi sawa cha pombe wanapata madhara sawa ya pombe.

UONGO

Ini huchakata pombe kupitia vimeng'enyo ambavyo vinaitwa Alcohol Dehydrogenase au ADH. Wanawake wana ADH chache zaidi mwilini mwao. Hii ina maana kwamba wanaweza kunywa kiasi hicho hicho lakini wakapata madhara zaidi kuliko wanaume.

SWALI LINGINE

Watoto wanaweza kunywa kidogo ili wajifunze kunywa kistaarabu watakapo kuwa wakubwa.

UONGO

Watoto na watu walio chini ya umri, hawaruhusiwi kunywa pombe au vileo. Kuna madhara mengi yanayohusishwa na unywaji wa pombe katika umri mdogo ikiwa ni pamoja na kuathiri ubongo wako, kuongeza hatari ya afya ya akili, kupata sumu inayotokana na pombe, ajali na majeraha.

SWALI LINGINE

Unywaji wa pombe au vileo kabla kuendesha gari unaweza kuleta madhara gani?

Haya yote

Unywaji wa pombe au vileo kabla kuendesha gari huathiri maamuzi, utambuzi na maono yako. Habari njema ni kwamba unywaji wa pombe au vileo na kuendesha gari unaweza kuzuilika kabisa. Jiunge na kampeni ya #jointhepact kwa kuchagua 'NDIO' sitakunywa na kuendesha gari.

NDIO Sina uhakika

Je, kunywa bia kunaleta afya zaidi kuliko wine (mvinyo) ama pombe kali?

UONGO

Kiasi cha kawaida cha pombe kali, bia au wine (mvinyo) huwa sawa katika kila kipimo. Kiasi cha kawaida cha pombe kwa ujumla ni kama 10-15ml. Athari za pombe mwilini huchangiwa na kiasi unachokunywa na sio kile unachokunywa.

SWALI LINGINE

Ukichanganya bia, wine (mvinyo) na pombe kali unalewa haraka zaidi.

UONGO

Huu ni mtizamo wa kawaida. Pombe ni pombe hata kama ni bia wine (mvinyo) au pombe kali. Madhara yake huchangiwa na kiasi unachokunywa na sio kile unachokunywa.

SWALI LINGINE

Kama unataka kupunguza virutubisho kwenye kinywaji chako, kunywa wine tu. Bia na pombe kali husababisha unene.

UONGO

Kuna takribani virutubisho mia mbili katika glasi ya ujazo ya 200ml ya wine. Ukilinganisha na kipimo cha 30ml cha pombe kali ambacho kina virutubisho takribani 50 na chupa ya bia yenye ujazo wa 330ml ambayo inavirutubisha takribani 150. Kumbuka, virutubisho kwenye kinywaji chako kinategemea ukali wa pombe, kiasi na vitu vingine vinavyo changanywa ili kuongeza ladha.

SWALI LINGINE

Kabla ya kunywa unatakiwa…

Vyote viko sawa

Kula chakula na kunywa maji muda wote unapokunywa pombe. Kula chakula kunapunguza kiasi cha pombe kinachoingia kwenye damu yako kwa kukihifadhi tumboni kwako muda mrefu. Kunywa maji kunasaidia mwili wako kuwa vizuri. Kila wakati unapokunywa pombe, panga namna ya kurudi nyumbani- usinywe pombe na kuendesha gari.

SWALI LINGINE

Inachukuwa muda gani kwa ini lako kuchakata kipimo kimoja cha pombe kali?

Lisaa limoja

Inachukuwa takribani lisaa limoja kuchakata kipimo cha kawaida.

SWALI LINGINE

Je, unafikiri kwa sasa unajua zaidi kuhusu pombe na madhara yake kwa mwili?

Je, ungependa kushiriki tena?

Toa tathmini yako

Maoni yako?

How interesting did you find these questions?
TUMA

Je, ungependa kushiriki tena?